Videos

Watoto 3 wafariki kutokana na moto eneo la Pipeline, NakuruWatoto watatu pamoja na yaya wao wamefariki kufuatia mkasa wa moto uliotokea eneo la Pipeline, kaunti ya Nakuru. Inaaminika kuwa moto huo ulisababishwa na mshumaa uliokuwa ukiwaka kwenye nyumba walimokuwa.
Kwa mujibu ya walioshuhudia, familia hiyo ilikuwa imehamia nyumba hiyo siku chache zilizopita, na ilikuwa na hitilafu ya nguvu za umeme, na hivyo kulazimika kutumia mishumaa baada ya juhudi za kununua umeme kuambulia patupu. Naibu kamanda wa polisi wa Nakuru Phanton Analo akisema kuwa, polisi walifika eneo la mkasa na kupata waathiriwa wameshafariki. Mama wa nyumba hiyo alikuwa kazini wakati wa mkasa huo.

source

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *